TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI.

Na Estom Sanga -TASAF

Menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF imekutana na Wadau wa Maendeleo kujadili masuala mbalimbali ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani kaya Milioni Moja na Laki Moja nchini kote.

Akitoa taarifa katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bwana Ladislaus Mwamanga amesema hatua kubwa imepigwa katika utekelezaji wa Mpango huo huku akiishukuru Serikali na Wadau wa Maendeleo kwa kuendelea kutoa msaada muhimu katika kufikia mafanikio hayo.

Aidha Bwana Mwamanga amesema msaada wa Serikali na Wadau wa Maendeleo unaoendelea kutolewa umeusaidia kwa kiwango kikubwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF kuandaa kwa ufanisi Awamu ya Pili ya Mpango huo inayotarajiwa kuanza hapo mwakani.

Amesema maandalizi hayo yanazingatia kwa kiwango kikubwa maelekezo ya Serikali yanayosisitiza umuhimu wa walengwa kufanya kazi za uzalishaji mali ili hatimaye waweze kuondokana na umaskini na kuboresha maisha yao.

Bwana Mwamang... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More