TASAF YANG’ARA MAONYESHO YA NANE NANE MKOANI SIMIYU. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TASAF YANG’ARA MAONYESHO YA NANE NANE MKOANI SIMIYU.

NA Estom Sanga –SIMIYU 
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeibuka mshindi wa pili katika kundi la Mifuko ya Jamii kwenye Maonyesho ya NANE NANE yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu kwa mwaka 2018/2019. 
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa ndiye aliyemwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika sherehe hizo za NANE NANE kuwakabidhi zawadi washindi mbalimbali ukiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF. 
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii katika banda lake kulikuwa na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao wameonyesha bidhaa mbalimbali wanazozitengeneza baada ya kupata ruzuku kutoka TASAF kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. 
Miongoni mwa bidhaa zilizoonyeshwa na Walengwa hao wa TASAF ni pamoja na mkaa wa kupikia walioutengeneza kwa kutumia udongo wa Mfinyanzi na vumbi la mkaa,dagaa,vikapu mazuria ya kufutia vumbi,pochi na vikapu vilivyotengenezwa mwa shanga,nguo zilizoshonwa kwa cherehani,cheni na mapambo ya wanawake. 
Akizungumza baada ya k... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More