TAWA yawakamata,wapokonya baiskeli 60, Nyaya 100 za majangiri - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAWA yawakamata,wapokonya baiskeli 60, Nyaya 100 za majangiri

NA RIPOTA WETU,KILOMBEROMAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), katika kipindi cha mwaka 2017/18 imekamata baiskeli 60 za watuhumiwa wa ujangiri zikiwamo Nyaya zaidi ya 100 ndani ya Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi- Msolwa.
Mkuu wa Kanda hiyo, Augustine Ngimilanga alisema pamoja na kukamata nyenzo hizo askari wa doria pia walikamata watuhumiwa wa ujangiri waliofunguliwa kesi 92 zinazoendelea Mahakama ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
“Watuhumiwa 18 wameshasomewa kesi zao na kuhukumiwa baadhi wamefungwa miaka mitatu na wengine miaka tisa jela,” alisema Ngimilanga na kuongeza:
“Tumeweka mkakati wa kuhakikisha maeneo yote yanakuwa na ulinzi wa doria muda wote, hii ni pamoja na kukabiliana nao kabla hawajaingia na kufanya uharibifu,” alisema.

 Mofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), katika Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi -Msolwa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Kijiji cha Msolwa Station Kilombero mkoani ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More