TCCIA YAJIVUNIA UWEPO WAKE NA MCHANGO WALIOUTOA KWA MIAKA 30 KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI KWA KUSAIDIANA NA SERIKALI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TCCIA YAJIVUNIA UWEPO WAKE NA MCHANGO WALIOUTOA KWA MIAKA 30 KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI KWA KUSAIDIANA NA SERIKALI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
CHAMA cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo kinajiandaa kusheherekea miaka 30 tangu kuanzishwa kwake huku kikijivunia mafanikio ambayo yamepatikana katika sekta ya kilimo,biashara na viwanda kutokana na uwepo wao nchini.

Kimeeleza namna ambavyo kimeshiriki kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini n katika kipindi hiki cha kusheherekea miaka 30 ya uwepo wao kabla ya kufikia siku ya kilele Novemba mwaka huu watafanya shughuli mbalimbali katika wilaya na mikoa yote nchini.

Akizungumza Dar es Salaam Kaimu Rais wa TCCIA Octavian Mshiu amesema uwepo wao na mchango wake kwa Taifa mbali na kuwaunganisha vyombo mbalimbali vinavyojihusisha na kilimo,viwanda na biashara wamefanikisha uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji.

Amesema kimsingi huko nyuma watanzania walikuwa hawashiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi lakini kupitia TCCIA watanzania wameweza kushiriki kwa kuanzisha viwanda na kampuni na hivyo kuwa sehemu ya wawekezaji nchini."Kuna m... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More