TCRA:HAKIKISHENI TAARIFA MNAZOZITOA WAKATI WA KUSAJILI KADI ZENU ZA SIMU NI SAHIHI, VINGINEVYO SHERIA ITAFUATA MKONDO WAKE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TCRA:HAKIKISHENI TAARIFA MNAZOZITOA WAKATI WA KUSAJILI KADI ZENU ZA SIMU NI SAHIHI, VINGINEVYO SHERIA ITAFUATA MKONDO WAKE

Na. Vero Ignatus Arusha. 
Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imewataka wananchi kufahamu wajibu na haki zao wanazostahili  kupata kutoka kwenye mitandao inayotoa  huduma za mawasiliano sambamba na kutambua wajibu walionao kama watumiaji wa huduma za mawasiliano
Kaimu mkuu wa Kanda ya kaskazini Francis  Msungu amesema kuwa mamlaka inatoa elimu kwa wananchi kuzijua haki zao kutokana na mabadiliko yanayotokea ni mengi ya sayansi na teknolojia pamoja na maendeleo ya matumizi ya vifaa vya mawasiliano katika mitandao ya simu.
Amesema kwa sasa kumezuka wimbi la utapeli kupitia simu za mikononi,  hivyo wananchi  wametakiwa kuwa na tahadhari kubwa, wasikubali kurubuniwa katika vitu ambavyowanafahamuhawajashiriki Usitekeleze maagizo yeyote yahusuyo fedha kwa ujumbe wa maandishi,
"Mfano unatumiwa ujumbe kuwa umeshinda bahati na sibu katikaMashindano ambayo hujashiriki, ukipokea ujumbe umetumiwa pesa na mtu usiyemfahamu usizitoe fedha hizo, hadi  uthibitishe ya kwamba zimetumwa kwa nia nzuri" 
A... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More