TCRA Kanda ya Mashariki yakutana kujadili huduma za mawasiliano - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TCRA Kanda ya Mashariki yakutana kujadili huduma za mawasiliano

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa changamoto ya mawasiliano ni watumiaji wenyewe kwa kutojua namna ya kutumia mitandao.

Odiero aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa Kanda ya Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa mkutano wa wadau ni kutaka kupata ushauri na changamoto ya mawasiliano katika utoaji huduma unaofanywa na TCRA Kanda ya Mashariki.

Mhandisi Odiero amesema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wadau ikiwa ni utoaji wa maoni pamoja na changamoto zinazowakabili ambazo baada ya mkutano huo zitashugulikiwa.  Aidha amesema kuwa mkutano huo ni pamoja na kujua mkataba wa TCRA katika utoaji huduma ikiwa na watoa huduma kutoa mkataba kwa wateja wao kwa bidhaa wanazozipata.

Odiero amesema kuwa malalamiko walioyapokea ni 57 ambapo wanashughulikia  yanayohusiana na matumizi ya simu. Mmoja wa wadau meneja wa Abood Media Abeid Dogori ames... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More