TCRA KANDA YA ZIWA YAFAFANUA KWA MADIWANI KUHUSU MAUDHUI YA CHANELI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TCRA KANDA YA ZIWA YAFAFANUA KWA MADIWANI KUHUSU MAUDHUI YA CHANELIMKUU wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ametoa wasilisho la chaneli za maudhui ya bila kulipia kwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato. Akizungumza mbele ya madiwani hao leo Mhandisi Mihayo amewaambia madiwani hao mkakati wa TCRA ni kuhakikisha wenye visambusi wanafuata leseni zao ili kutoa fursa kwa Watanzania kupata haki ya kuona chaneli kama ambavyo leseni zinavyoelekeza. Hivyo amewataka madiwani hao kuwaeleza wananchi kuhusu visambusi ambavyo wanatakiwa kununua na ili kuona chaneli zote muhimu bila kulipia. 
 "Madiwani wetu tunawaomba muwaambie wananchi wanunue visambusi vya TING, DigTeck,Startimes na Contineto ambavyo ndivyo vyenye leseni ambazo zinawapa uhalali wa kuonesha chaneli za nyumbani,"amesema Mhandisi Mihayo. Amefafanua baada ya kuona kuna wamiliki wa visambusi wanakiuka taratibu ilifunguliwa kesi mahakamani na baada ya kushinda wakaona ni vema watu wakaumia alau kidogo lakini kurudisha ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More