TCRA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamekamata watu 14 wanaondesha usajili laini simu - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TCRA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamekamata watu 14 wanaondesha usajili laini simu

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendesha operesheni wahudumu 14 wanaosajili watu kwa kutumia alama za vidole bila kuwa na vitambulisho vya watoa huduma vya Kampuni za simu.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa waliokamatwa wanatakiwa mashitaka kutokana na kutumia mashine za kusajili alama za vidole bila kuwa kitambulisho cha mtoa huduma Kampuni ya simu husika.
Operesheni hiyo leo imeendeshwa katika Kanda zote za TCRA kwa watu wanaoendesha usajili wa alama za vidole bila kuwa vitambulisho vya watoa huduma.

Amesema ni kosa la kisheria kuendesha usajili wa laini za simu bila kuwa na kitambulisho na kuongeza kuwa baadhi yao wanafanya udanganyifu kwa wananchi kwa kuwatoza fedha.
Amesema mawakala waliowapa mashine  hizo wamefanya kosa la kisheria kwa utoaji wa mashine hizo kiholela.

Mhandisi Odiero amesema walishatoa namna ya usajili hivyo lakini baadhi wamekiuka utarati... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More