TEAM SAMATTA YAILAZA 4-2 TEAM KIBA, AJIBU AFUNGA MAWILI…BOBAN ANG’ARA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TEAM SAMATTA YAILAZA 4-2 TEAM KIBA, AJIBU AFUNGA MAWILI…BOBAN ANG’ARA

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
TIMU ya mwanasoka Mbwana Ally Samatta na Rafiki zake imefanikiwa kushinda mabao 4-2 dhidi ya mwanamuziki Ally ‘King’ Kiba na Marafiki zake katika mchezo maalum wa kirafiki wa Hisani uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa wa zamani wa kimataifa wa FIFA, Osman Kazi, Team Kiba ilitangulia kwa mabao ya mshambuliaji wa Yanga SC, Ibrahim Ajibu Migomba dakika za tatu na 30, kabla ya Team Samatta kuzinduka na kusawazisha yote ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Na mabao yote yalitokana juhudi za ndugu wa damu, watoto wa mzee Ally Samatta, Mohammed anayechezea Mbeya City na mdogo wake Mbwana wa KRC Genk ya Ubelgiji.
Mbwana Samatta (kulia) akitafuta maarifa ya kumpita beki kizingiti wa Team Kiba, Mohammed Bin Slum (kushoto) 
Ibrahim Ajibu wa Team Kiba (kulia) akipambana na Super Jamhuri Kihwelo (chini) wa Team Samatta 
Haruna Moshi 'Boban' wa Team Samatta (kulia) akiambaa na mpira baada ya kuwatoka mabeki wa ... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More