Teknolojia ya Kitalu Nyumba Kuwakomboa Vijana - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Teknolojia ya Kitalu Nyumba Kuwakomboa Vijana

Serikali imejipanga kuboresha upatikanaji wa ajira kwa vijana nchini kupitia teknolojia ya kilimo cha kisasa (Green house).  
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Mkoa wa Songea na Iringa ili kuhamasisha na kukagua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kujenga vitalu nyumba (Green house) kwenye Mikoa hiyo.
Waziri Mhagama alisema kuwa Serikali imeamua kuanzisha mradi huo ili kuhakikisha vijana wanafikiwa kwa idadi kubwa na kuwawezesha kupata ujuzi na ajira kupitia teknolojia ya kilimo cha kisasa itakayowawezesha kujipatia kipato.
“Teknolojia hii itawawezesha vijana kulima katika eneo dogo, kupata mazao kwa wingi na kuweza kuyauza, vilevile kutumia eneo hilo kuweza kuajiri vijana wengine kwani asilimia zaidi ya 60% ya watu wanaojiajiri na kujishughulisha inatokana na na mashamba.” alisema Mhagama
Ameongeza kuwa vijana watafundishwa teknolojia hiyo ya kilimo cha kitalu ny... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More