TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI

Na Mwamvua Mwinyi, FUKAYOSI BAADHI ya wakulima kitongoji cha Segwa, kata ya Fukayosi Bagamoyo mkoani Pwani, kinakabiliwa na tatizo la uvamizi wa tembo ambao wameharibu mazao yao kwenye hekari kumi na kuvunja nyumba mbili. 
Akielezea kero hiyo wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dk.Shukuru Kawambwa, katika kata ya Fukayoso, mwenyekiti wa kijiji cha Mwavi,Shabani Mkumbi alisema ,tembo wamekuwa wakitokea hifadhi ya Taifa Saadani na kuvuka mto WAMI na kuingia katika maeneo ya watu kwenye vijiji vya Fukayosi  na Mwavi . 
"Mazao yaliyoharibiwa ni muhogo ,matikiti,nyanya Maji ,nyanya chungu,maboga , hoho, mananasi, migomba na miwa ." alisema. Mkazi wa Segwa Hassan Kalahuka alisema ,kutokana na tatizo hilo wameamua kuunda kamati ambayo itafuatilia suala la fidia kupitia ofisi ya wilaya kwani wao wamekwama. 
Mmoja wa aliyeathiriwa shamba lake na tembo hao ,Ramadhani Mfaume alielezea ,mbali ya kuharibiwa mazao yake pia gunia zake kumi zimeharibiwa. 
Alibainisha tangu apate hasara ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More