Tetema ya Rayvanny imekosa uhalisia, Mtoto wangu namuandalia mazingira kuja kuwa Rais – Beka Flavour - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tetema ya Rayvanny imekosa uhalisia, Mtoto wangu namuandalia mazingira kuja kuwa Rais – Beka Flavour

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Beka Flavour amesema kuwa wimbo wa Tetema wa Rayvanny umekosa uhalisia kwani pale alipotumia misemo maarufu inayotumiwa na Piere Likwidi ya “Aaahh mama shigidi aah, Nakufa wooi wicked aahh Aahh mama shigidi konki Fire, moto, liquidy” alitakiwa amuweke Piere ili iwe na uhalisia kwani ndiye aliyebuni misemo hiyo.Beka ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya ‘Lamba Lolo’ amesema kuwa anaamini wimbo wake huo ambao amemshirikisha Piere Likwidi ni moja ya nyimbo zake kubwa zilizopokelewa vizuri.


Kwa upande mwingine, Beka Flavour amesema kuwa anamuandalia mtoto wake Aaryan kuja kuwa Rais wa Tanzania kwani anaamini akimsomesha vizuri kila kitu kinawezekana.


The post Tetema ya Rayvanny imekosa uhalisia, Mtoto wangu namuandalia mazingira kuja kuwa Rais – Beka Flavour appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More