Tetesi za Kayumba kutoka kimapenzi na Irene Uwoya ‘Ikitokea nafasi najitosa’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tetesi za Kayumba kutoka kimapenzi na Irene Uwoya ‘Ikitokea nafasi najitosa’

Muimbaji Kayumba ambaye ni zao la shindano la BSS, hivi karibuni amekuwa akihusishwa na kashfa nzito ya kutoka kimapenzi na aliyekuwa mke wa Dogo Janja, Irene Uwoya.Tetesi hizo zilipamba moto mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2018 baada ya muimbaji huyo kum-wish birthday muigizaji huyo ujumbe ambao ulitafsiriwa za kiahaba.

Baada ya tetesi hizo kukuwa kila siku, Muimbaji huyo alibambwa na HZB alieleza kinaga ubaga mahusiano yake na mrembo huyo ambaye anatawa katika mitandao ya kijamii kutokana na mikato yake ya mavazi.

“Najisikia tu kiandika kuhusiana na Irene hata yeye huwa ananijibu,” alisema Kayumba.

Aliongeza, “Hata unapomuona anaimba nyimbo zangu anapenda muziki mzuri, kwahiyo amekutana na muziki nzuri kwangu. Kama zikitokea ishu za mahusiano hatuwezi kuzizuia,”

Mremboo huyo kutoka kiwanda cha filamu, amekuwa akihusishwa kuachana na rapa Dogo Janja lakini hakuna mmoja kati yao aliyewahi kuthibitisha hilo.


The post Tetesi za Kayumba kutoka kimapenzi na Irene... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More