Tetesi za usajili barani Ulaya Jumapili 10.06.2018 - Sports Kitaa | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumapili 10.06.2018


Kiungo wa Dortmund na Ujerumani Mario Gotze 26 hawezi kuacha kufikiri uwezekano wa yeye kuungana na kocha wa liverpool Jurgen klopp ambaye aliwahi kuifundisha dortmund (DAZN, via Independent)

Lyon wame achana na mpango wa kumuuza Nabil Fekir Kwa liverpool baada ya majogoo hao wa anifield kutaka kumpata kiungo huyo raia wa ufaransa Kwa bei pungufu ikiwa ni baada ya kufanyiwa vipimo vya Afya. (Sunday Mirror)

Liverpool ina mapango wa kumchukua mlinda mlango wa Burnley na England Nick Pope kwa pauni milioni 15.(Sun on Sunday)

Meneja wa Celtic Brendan Rodgers anatazamiwa na Leicester City kuwa huenda akamrithi Claude Puel. (Sun on Sunday)

Real Madrid imempatia mshambuliaji Cristiano Ronaldo mkataba wa thamani ya pauni milioni 28.5 kwa mwaka lakini huenda kisiwe kitita cha kutosha kwa mchezaji huyo . (Cadena COPE, via Sunday Express)Cristiano Ronaldo

Winga wa Stoke, Xherdan Shaqiri, 26, ameendelea kusita, bado hajafanya maamuzi ya kuhamia Liverpool. (Metro)

Arsenal wako tayari kusaka saini Kiungo mkabaji wa Sampdoria raia wa uruguai mwenye miaka 22 Lucas Torreira. (Calciomercato Sampdoria, via Star on Sunday)

Manchester City wanaweza hamishia macho Kwa kiungo wa Nice raia wa Ivorycost Jean Michael Seri 26 baada ya dau Lao la pauni million 60 kwa Jorginho raia wa italia kukataliwa. (Sunday Mirror)

Manchester United imekuwa ikimtolea macho mshambuliaji wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic lakini mchezaji huyo mwenye miaka 23 amesema ataamua timu ya kuchezea baada ya Kombe la dunia.(Mail on Sunday)Sergej Milinkovic-Savic ataamua klabu ya kuichezea baada ya kombe la dunia la nchini Urusi

Tottenham inafikiria kumchukua mchezaji wa miaka 22 wa Aston Villa na mchezaji wa england wa kikosi cha umri wa miaka 21, Jack Grealish.(Sky Sports)

Wolves wanajiimarisha baada ya kurejea ligi kuu , wameonyesha ya kumtaka mlinzi Imrane Bouchema Raia wa ufaransa mwenye miaka 18 ambaye yuko huru baada ya kumaliza mkataba wake na Tours.(L'Equipe, via Birmingham Mail)

West Brom inajiandaa na michuano ya mabingwa kwa kufanya usajili wa mshambuliaji Bobby Reid 25, wa Bristo City kwa kitita cha pauni milioni 10 na kiungo wa St Kitts and Navis Romaine Sawyers 26. (Sunday Telegraph)

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah hajamsamehe nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos baada ya kuumizwa kulikomsababishia kuondoka uwanjani wakati wa fainali ya ligi ya mabingwa.(Marca, via Mail on Sunday)


Source: Sports KitaaRead More