TFDA yajivunia kuipaisha Tanzania kwa kuwa na mifumo bora ya udhibiti,kuifanya nchi ya kwanza barani Afrika kufikia hatua hiyo - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TFDA yajivunia kuipaisha Tanzania kwa kuwa na mifumo bora ya udhibiti,kuifanya nchi ya kwanza barani Afrika kufikia hatua hiyo

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema katika kipindi Cha Miaka mitatu imefanya mambo mbalimbali ya udhibiti wa usalama, ubora na usalama wa bidhaa za ndani na nje ya Nchi ikiwemo kutambulika kimataifa kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya ISO 9001: 2015.
Hii ni kutokana na mafanikio ya miaka mitatu ya utekelezaji wa kazi chini ya Serikali ya Awamu ya Tano, kwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Adam Fimbo amebainisha hayo wakati akitoa ripoti ya miaka mitatu ya Mamlaka hiyo wakati wa ziara maalum ya Maafisa Mawasiliano na habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kampeni maalum ya ‘Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.
"Kutokana na kuwa na mifumo thabiti ya udhibiti wa... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More