TFDA YATOA ELIMU YA MADHARA YA SUMUKUVU KWA WASINDIKAJI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TFDA YATOA ELIMU YA MADHARA YA SUMUKUVU KWA WASINDIKAJI


Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA kanda ya Kati Dodoma imeanza kutoa elimu kwa wasindikaji wa mazao ya Nafaka baada ya kubaini baadhi ya bidhaa wanazozalisha hususani unga wa mahindi na siagi ya karanga kuwa na vimelea vya ugonjwa wa sumukuvu ambao ni hatari kwa afya ya watumiaji na wakati mwingine husababisha vifo. 
Mafunzo hayo yanatokana na ripoti ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa bidhaa zitokanazo na unga mchanganyiko na siagi ya karanga uliofanywa na mamlaka hiyo ya mwaka 2015-2018 na kubaini mazo hayo huzalishwa kwa wingi mkoani humo yana dalili ya uwepo wa fangasi na sumukuvu. 
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya kati DK.Englbert Bilashoboka amesema kuwa  Mamlaka imeanza kutoa elimu kwa wasindikaji wa mazao ya Nafaka baada ya kubaini baadhi ya bidhaa wanazozalisha hasa Unga wa Mahindi na Siagi ya Karanga kuwa na vimelea vya ugonjwa wa Sumukuvu.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Maduka Kessy amesema kuwa ugonjwa huo hu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More