TFF WAACHANE NA YANGA, WAICHUKUE SINGIDA UNITED KAMA LENGO NI TANZANIA IFANYE VIZURI KOMBE KA KAGAME - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TFF WAACHANE NA YANGA, WAICHUKUE SINGIDA UNITED KAMA LENGO NI TANZANIA IFANYE VIZURI KOMBE KA KAGAME

Na Winchislaus Josephath
NIMEKUWA msomaji wa makala zako to unaandika kwenye blog hadi leo hii kwenye website. Shida tu ni moja kwamba website yako hairuhusu comments kwenye makala zako. 
Ila nikupongeze kwamba mara zote umekuwa ukisimamia ukweli.
Nia yangu leo ni kujaribu kuhoji juu ya nafasi ya TFF tuliyonayo sasa kusaidia vilabu vya nyumbani kufanya vizuri kwenye michuano wanayoshiriki.
Kwa mfano, najiuliza TFF wana malengo gani na michuano ya Kagame? wanapeleka timu ili zikashiriki au tunapeleka timu zikashindane? Yanga wamejitathmini na wamegundua hawana timu ya kushindana, unawezaje kuwalazimisha washiriki? au timu inavyofungwa na kutia aibu, TFF wanafaidika na nini? 

Kila mtu anajua kuwa wachezaji Yanga hawajalipwa mishahara wala posho zao kwa kipindi kirefu. Kila mtu anajua kuwa Yanga hata Ligi wamemaliza kwa kubahatisha hadi wanakula kwa mama ntilie kwa kukOsa hela za maandalizi.
Kila mtu anajua kuwa sasa hivi Yanga haina kocha maana, Nsajigwa vyeti vyake havimruhusu kukaa benchi ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More