TFF yaazimia kuweka historia mpya katika soka - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TFF yaazimia kuweka historia mpya katika soka

Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) limetamba kwamba baada ya kuitupa nje ya timu ya Burundi katika michuano ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar, sasa inaelekeza nguvu kwenye michezo mitatu inayofuata, ili ushindi upatikane na hatimaye kuwa nafasi nzuri ya kuweka historia mpya katika soka. 
tanza

Katibu Mkuu Mtendaji wa TFF, Wilfred Kidao amesema, azma hiyo haitaishia katika kutafuta nafasi ya kucheza fainali ya kombe la dunia pekee, bali pia kupata mafanikio kama hayo kwa Michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) ambapo Tanzania imepangwa kucheza na dhidi ya Sudan.


Kidao anasema mafanikio hayo yatakuwa chachu ya kujenga historia mpya katika uga wa soka nchini, na kuendeleza furaha kwa mamilioni ya Watanzania. 


Haji Manara na Steve Nyerere ni miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya hamasa ya saidia timu ya taifa ishinde, na baada ya matokeo ya Stars na Burundi, leo wamewatolea uvivu mashabiki wanaokwenda uwanjani na kushangilia baadhi ya mat... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More