TFF YABADILI MFUMO WA LIGI KUU NA LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TFF YABADILI MFUMO WA LIGI KUU NA LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imebadili kupitisha mfumo wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara juu ya timu za kushuka na kupanda.
Na kuanzia msimu ujao FDL itachezwa katika makundi mawili yenye timu 12 na timu 1 kutoka kila kundi itapanda kwenda Ligi Kuu wakati timu zitakazoshika nafasi ya pili na ya tatu katika makundi yote zitacheza mtoano kwa mechi za nyumbani na ugenini.
Taarifa ya TFF imesema kwamba washindi katika mechi hizo watacheza na timu zilizoshika nafasi ya 17 na 18 katika Ligi Kuu kupata timu mbili zitakazocheza Ligi Kuu, huku timu mbili za nafasi ya 19 na 20 zikishuka daraja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akisalimiana na wachezaji wa Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba Mei 19, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Timu hizo mbili za Ligi Kuu zilizoshika nafasi ya 17 na 18 kama zitapoteza michezo yao zitashuka Daraja kuungana na zilizosh... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More