TFF YASISTIZA HAITAMBUI UENYEKITI WA MANJI YANGA SC NA ANATAKA ACHUKUE FOMU AGOMBEE KWENYE UCHAGUZI WA JANUARI 13 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TFF YASISTIZA HAITAMBUI UENYEKITI WA MANJI YANGA SC NA ANATAKA ACHUKUE FOMU AGOMBEE KWENYE UCHAGUZI WA JANUARI 13

Na Nasra Omary, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la  Soka Tanzania (TFF), Malangwe Mchungahela amesema kwamba hawamtambui Yussuf Manji kama  Mwenyekiti wa Yanga.
Hayo yamekuja mara baada ya wajumbe wa kamati  ya utendaji walipokutana na mwenyekiti huyo huku  wakiwa na hoja ya kukubali kufanya uchaguzi  isipokuwa nafasi ya uwenyekiti.
Mchungaha alisema kuwa kwa mujibu wa katiba ya  Yanga, ibara ya 28 kanuni ya tatu (c) inasema mjumbe  atakoma kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji iwapo  atashindwa kutekeleza majukumu ya mjumbe  kutokana na kuumwa au sababu nyingine yoyote kwa  kipindi cha miezi 12 mfululizo.

TFF Imesema haItambui Uenyekiti wa Yussuf Manji Yanga SC na akitaka kuendelea kuwa kiongozi wa klabu hiyo agombee

Katiba hiyo ya marekebisho ya mwaka 2010, ibara ya  14 inamruhusu mwanachama yoyote kujiuzulu na  kuwasilisha barua kwa katibu mkuu wa Yanga kwa barua ya rejesta.
Mchungahela alisema kuwa hawamtambui Manji  kama mwenyekiti wa Yanga kama kat... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More