TFF YAWAAGIZA YANGA SC KUFANYA UCHAGUZI WA KUZIBA NAFASI ZA MANJI, SANGA NA WAJUMBE WANNE JANURI 13 MWAKANI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TFF YAWAAGIZA YANGA SC KUFANYA UCHAGUZI WA KUZIBA NAFASI ZA MANJI, SANGA NA WAJUMBE WANNE JANURI 13 MWAKANI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Yanga SC kufanya Uchaguzi wa kuziba nafasi za viongozi wake waliojiuzulu ifikapo Januari 13 mwakani, 2019.
Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Malangwe Mchungahela amewaambia Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam kwamba Yanga inatakiwa kuanza mchakato wa uchaguzi wake ambao lazima ufanyike Januari 13, 2019.
Mchungahela amezitaja nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huo ni za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.
Na hiyo inafuatia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuiagiza Yanga kuitisha uchaguzi wa kujaza nafasi za viongozi waliojiuzulu ili kuwa na safu imara ya uongozi.

Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Malangwe Mchungahela ameitaka Yanga kufanya uchaguzi wake  Januari 13 mwakani

Kwa mujibu wa kalenda ya Uchaguzi, Novemba 5 hasi 7, 2018 Yanga watatakiwa kutangaza mchakato wa Uchaguzi na kubandika kwenye mbao za matangazo, zoezi ambalo litafanywa na Mw... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More