Thiery henry akabidhiwa mikoba ya Leonardo Jardim , baada ya Mvenezuela huyo kutimuliwa - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Thiery henry akabidhiwa mikoba ya Leonardo Jardim , baada ya Mvenezuela huyo kutimuliwa

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Thiery Henry amekabidhiwa mikoba ya Mvenezuela Leonardo Jardim baada ya kutimuliwa katika klabu ya AS Monaco kutoka Ufaransa.


Henry kabla ya kuchukua mokoba ya Leonardo Jardim alikuwa akiinoa timu ya taifa ua Ubelgiji akiwa kama kocha msaidizi chini ya Robero Martinez kuanzia mwaka 2016 hadi hivi sasa.


Mfaransa huyo ameisaidi timu hiyo ya Ubelgiji kufika hatua nusu fainali na kuchukua nafasi ya tatu katika michuano mikubwa kabisa ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Urussi 2018.


Leonardo Jardim ameifundisha Monaco kwa takribani misimu minne kuanzia mwaka 2014 hadi hivi sasa 2018,huku akiisaidia kutwa taji la ligi kuu nchini Ufaransa msimu 2016/17.

By Ally Juma.


The post Thiery henry akabidhiwa mikoba ya Leonardo Jardim , baada ya Mvenezuela huyo kutimuliwa appeared first on Bongo5.com.

... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More