Tigo Wazindua Malipo ya kielekroniki Serikalini Arusha - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tigo Wazindua Malipo ya kielekroniki Serikalini Arusha

KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (Auwasa) wamezindua mfumo mpya wa malipo ya kielekroniki serikalini (GePG) katika mikoa ya Arusha , Kilimanjaro na Manyara.

Mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa Ankara mbalimbali pamoja na kufanya malipo kutokana na huduma wanazopata kutoka taasisi za serikali zaidi ya 300 lengo ikiwa ni kurahisisha watumiaji wa huduma kutokaa katika misururu. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua mfumo huo , Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Nancy Bagaka alisema kuwa mfumo huo utapunguza kwa kiwango kikubwa ubadhirifu jambo ambalo litaongeza mapato ya serikali.

“Kutokana na mfumo huu faida nyingi zitapatikana ikiwemo kuongeza mapato ya serikali kupitia taasisi na mashirika , kuboresha uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu , utoaji taarifa za mara kwa mara pamoja na kuondoa ubadhirifu na wizi” alisema Bagaka. Aidha alisema ili kuweza kulipia Ankara mt... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More