TIGO YAZINDUA MTANDAO WA 4G+ TANZANIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TIGO YAZINDUA MTANDAO WA 4G+ TANZANIA

Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali Tigo Tanzania, leo imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za mtandao wenye kasi ya juu zaidi nchini baada ya kuzindua teknolojia ya 4G+. Uzinduzi wa mtandao wa 4G+ unathibitisha kuwa Tigo ni kampuni pekee ya mawasiliano inayofanya ubunifu unaoboresha huduma zake kuendana na mahitaji halisi ya wateja nchini kote.

‘Uzinduzi wa  4G+ ni sehemu ya safari ya mabadiliko ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo hapa nchini. Lengo letu ni kuwawezesha wateja kufurahia huduma bora zaidi za kidigitali. Daima tuko mbele katika kuleta teknologia za kisasa za mawasiliano nchini,’ Afisa Mkuu wa Tigo – Teknologia na Mawasiliano Jerome Albou aliwaambia waandishi wa habari katika uzinduzi wa mtandao wa Tigo 4G+ jijini  Dar es Salaam. 

Sasa wateja wa Tigo wanaweza kufurahia huduma bora, za uhakika na zenye kasi ya juu zaidi ya kupakua maudhui kutoka kwenye mtandao kwa gharama zile zile. Ili kufurahia mtandao wa 4G+, mteja anahitaji kuwa na simu yenye uwezo... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More