TP MAZEMBE YATOLEWA KWA MABAO YA UGENINI LIGI YA MABINGWA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TP MAZEMBE YATOLEWA KWA MABAO YA UGENINI LIGI YA MABINGWA

TIMU ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya robo Fainali tu kwa mabao ya ugenini.
Hiyo ni baada ya Mazembe kulazimishwa sare ya 1-1 na C.D. Primeiro de Agosto katika mchezo wa marudiano jioni ya leo Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi.
Mshambuliaji kinda wa miaka 20 wa DRC, Jackson Muleka aliifungia bao la kuongoza Mazembe mapema tu dakika ya 12, akimalizia pasi ya kiungo Muivory Coast,  Christian Raoul Kouame Koffi.

Lakini TP Mazembe ikashindwa kujilinda na kuwaruhusu wageni kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji Mkongo pia, Mongo Kipe Lumpala Bokamba dakika ya 34 akimalizia pasi ya mshambuliaji Muangola, Hermenegildo Costa Paulo Bartolomeu.
Na kwa sababu mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya 0-0 Jumamosi Uwanja wa Estádio 11 de Novembro mjini Luanda, Primeiro de Agosto inakwenda Nusu Fainali kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 1-1.... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More