TPDC YAKABIDHI KAMBI NAMBA 8 KWA SERIKALI YA KIJIJI CHA NJIA NNE WILAYA YA KILWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TPDC YAKABIDHI KAMBI NAMBA 8 KWA SERIKALI YA KIJIJI CHA NJIA NNE WILAYA YA KILWA

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kuimarisha huduma mbalimbali za kijamii kwa Vijiji na Mitaa inayoguswa na miundombinu ya bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. Katika kufikia azma hii TPDC imekabidhi kambi Namba 8 kwa kijiji cha Njia nne Wilayani Kilwa ili Kijiji kiweze kupanga matumizi sahihi ya Kambi hiyo.
Kukabidhiwa kwa majengo ya Kambi hayo kunatokana na kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya bomba la gesi asilia kutoka Madimba-Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam, hivyo kufanya majengo hayo kutotumika tena kwa shughuli za ujenzi. 
Akikabidhi rasmi kambi hiyo kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Njia nne hivi karibuni, Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TPDC Bi. Marie Msellemu alisema kuwa “Mikoa ya Lindi na Mtwara ni wadau wakubwa katika ustawi wa miundomibinu ya bomba la gesi asilia na tumekuwa tukishirikiana katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo na ya kijamii ikiwemo afya, michezo, utawala bora na maji lengo ikiwa ni k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More