TRA YAKAMATA BIDHAA MBALIMBALI KUPITIA NJIA ZA MAGENDO ZIKIWA NA THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 20 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TRA YAKAMATA BIDHAA MBALIMBALI KUPITIA NJIA ZA MAGENDO ZIKIWA NA THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 20

Na Veronica Kazimoto,Arusha
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekamata malori mawili yenye bidhaa mbalimbali eneo la Loliondo Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kupitia njia ya magendo yakitokea nchini Kenya zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20.
Akizungumza leo jijini Arusha, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere amesema kuwa, malori hayo yenye namba T 985 AJP na T 840 ABF yalikamatwa usiku wa Mei 10 2018 na kusisitiza kuwa wafanyabiashara wenye bidhaa hizo wamevunja sheria kwa kuwa hawakulipa kodi stahiki kama inavyotakiwa.
Kichere amefafanua kuwa, wafanyabiashara wenye bidhaa hizi zilizokamatwa, wamevunja kifungu cha sheria namba 82 na 200 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 na Sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2004. Hivyo kwa Sheria hizi, wafanyabiashara hawa wanatakiwa kulipa kodi pamoja na faini ya shilingi milioni 39 na magari yao kutaifishwa.
"Kwa ujumla bidhaa hizi zote zina thamani ya shilingi 20,037,330.15 ambayo kodi ya bidhaa hizi ni shilling... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More