TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.8 ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2018/19 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.8 ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2018/19

Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.84 kwa kipindi cha miezi mitatu ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai hadi Septemba, 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 3.65 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo amesema kiasi hiki ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.32 na kuongeza kuwa ukusanyaji wa mapato hayo umekuwa ukiongezeka kila mwezi.
“Katika mwezi Julai, 2018, TRA ilikusanya jumla ya shillingi trillioni 1.20 sawa na ukuaji wa asilimia 9.20, mwezi Agosti, 2018 jumla ya shilingi trillioni 1.27 zilikusanywa ikiwa ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.86 wakati mwezi Septemba, 2018 mamlaka ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.36 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.65,” alisema Kayombo.
Kayombo amewashukuru walipakodi wanaoendelea kulipa kodi zao kwa ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More