TRA YAKUSANYA TRILIONI 7.9 KATIKA KIPINDI CHA MIEZI 6 YA MWAKA WA FEDHA 2018/19 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TRA YAKUSANYA TRILIONI 7.9 KATIKA KIPINDI CHA MIEZI 6 YA MWAKA WA FEDHA 2018/19

Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 7.9 kwa kipindi cha miezi sita ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai hadi Desemba, 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 7.8 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo amesema makusanyo ya mwezi Desemba, 2018 yaliongezeka kuzidi makusanyo ya miezi yote iliyopita kwa mwaka huu ambapo TRA ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.63.
“Mbali na makusanyo hayo ya mwezi Desemba, katika mwezi Novemba, 2018 TRA ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.21 na mwezi Oktoba, 2018, zilikusanywa jumla ya shillingi trillioni 1.29. Nachukua fursa hii kuwashukuru walipakodi wote kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati”, alisema Kayombo.
Kayombo aliongeza kuwa, katika kutatua kero na malalamiko mbalimbali ya walipakod... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More