TRA YATANGAZA MSAMAHA WA MADENI YA RIBA NA ADHABU KODI ZA NYUMA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TRA YATANGAZA MSAMAHA WA MADENI YA RIBA NA ADHABU KODI ZA NYUMA


NA RACHEL MKUNDAI, DAR ES SALAAM.
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetangaza msamaha wa riba na adhabu za madeni ya nyuma ya Kodi hadi asilimia mia moja ili kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo kulipa kodi ya msingi tu yaani “Principal Tax”
Akitangaza msamaha huo, Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa msamaha huo ni matokea ya utekelezaji Maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Baraza la Wafanyabiashara (TNBC) uliofanyika Ikulu tarehe 20/03/2018 ambapo wafanyabiashara walilalamikia kuwepo kwa malimbikizo makubwa ya madeni ya kodi za nyuma yakijumuisha riba na adhabu,
Kichere amesema kuwa, ili kukamilisha hilo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefanya marekebisho kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2018 na sehemu ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015.
“Katika marekebisho hayo Waziri mwenye dhamana ya Fedha na Mipango amepewa mamlaka ya kutoa utara... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More