TRA YAWATAKA MAWAKALA FORODHA KUHAKIKISHA NAMBA ZAO ZA UTAMBULISHO WA MLIPAKODI (TIN) - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TRA YAWATAKA MAWAKALA FORODHA KUHAKIKISHA NAMBA ZAO ZA UTAMBULISHO WA MLIPAKODI (TIN)

Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imewataka Mawakala wa Forodha wote kuhakakisha wanafanya uhakiki wa namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza na kuisaidia mamlaka hiyo kukusanya mapato mengi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani wa mamlaka hiyo, Abdul Zuberi katika Semina iliyowakutanisha na makampuni ya mawakala wa forodha iliyojadili masuala mbalimbali ya kodi na ushuru wa forodha.
Amesema kuwa mawakala hao wanatakiwa kuhakiki TIN zao kutokana na kuwepo mkanganyiko kuwa na zaidi TIN hali inayowapa shida ya kutambua idadi ya mawakala wanaotakiwa kulipa kodi.“ Kuna watu wana TIN zaidi ya moja wanazitumia bila kufanyiwa uhakiki na wengine wanazifanyia udanganyifu inatupa tabu kuwatamabua hivyo ni vema mkazifanyia uhakiki,” amesema.
Amebainisha kuwa TRA mawakala watakaobainika kutumia TIN zaidi ya moja bila kuzifanyia uhakiki watachukuliwa hatua za kisheria.Amesisitiza kuwa mawakala wa forodha watakaofanya u... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More