TRC YAJIVUNIA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA RELI NCHINI , WASIFU JITIHADA ZA SERIKALI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TRC YAJIVUNIA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA RELI NCHINI , WASIFU JITIHADA ZA SERIKALI

Na Khadija Seif,Globu ya jamii
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema linajivunia kuboresha miundombinu ya reli nchini ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli kuboresha miundombinu hiyo ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa Standard Gauge Railways (SGR).
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa wakati anazungumzia miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk.John Magufuli ambapo amesema shirika hilo lina majukumu ya kutoa huduma za usafiri wa abiria wa treni za mikoani na treni za mizigo ndani ya nchi na nje.
Pia amesma kwa sasa TRC imerudisha safari ya treni ya mizigo kutoka Dar es salaam mpaka Mji wa Kampala nchini Uganda, ambapo ikiwa na miradi miwili ambayo ni mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na mradi wa uboreshaji wa reli ya kati pamoja na miradi midogo kama kurejesha njia ya Tanga, Arusha na... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More