TRENI YA KWANZA YA MWENDO KASI YAGONGA NG'OMBE NA KUPINDUKA - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TRENI YA KWANZA YA MWENDO KASI YAGONGA NG'OMBE NA KUPINDUKA


Treni ya kwanza ya mwendokasi nchini India imeanguka jana Jumamosi baada ya kugonga ng'ombe aliyekuwa kwenye reli, ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Mkuu Narendra Modi kuzindua huduma ya abiria.
Treni hiyo, Vande Bharat Express, ambayo inachukuliwa kuwa ni treni ya mwendo kasi kuliko zote nchini India na iliyojengwa chini ya kaulimbiu ya Serikali ya Modi ya "Make in India (Tengeneza Ndani ya india)", ilifanya safari yake ya kwanza Ijumaa ikitoka New Delhi kwenda Varanasi, ambao ni mji mtakatifu wa Hindu.
Lakini wakatio ikirejea kwenye mji huo mkuu wa India siku iliyofuata, iligonga ng'ombe na hivyo ajali hiyo kutibua ugavi wa umeme katika mabehewa manne na hivyo kuharibu breki, kwa mujibu wa Shirika la Reli la India.
"Baadaye treni ilipata matatizo ya kiufundi na hivyo kusimama wakati ikiwa njiani kwenda Delhi," msemaji wa shirika hilo, Smita Sharma aliiambia AFP.
Treni hiyo ilifika Delhi salama, ikiwa ni kabla ya kuanza safari za kibiashara leo, aliongeza.
Mifugo imekuwa tatizo kubwa katika bar... Continue reading ->Source: Mwanaharakati MzalendoRead More