Trump ataka Urusi irejeshwe kundi la G8 - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Trump ataka Urusi irejeshwe kundi la G8

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa wito mpya wa kuirudhisha Urusi katika kundi la mataifa yaliostawi zaidi kiviwanda duniani, licha ya kukumbana na upinzani mkali kwa pendekezo lake kutoka kwa wenzake nchini Canada.
"Nadhani ingekuwa jambo la manufaa kuirejsha Urusi," Trump aliwaambia waandishi habari kabla ya kuondoka kwenye mkutano wa kilele wa kundi la mataifa saba yalioendelea zaidi kiviwanda.
"Nadhani ingekuwa vizuri kwa Urusi, Nadhani lingekuwa jambo zuri kwa Marekani, nadhani ingekuwa vizuri kwa mataifa yote ya kundi la sasa la G7. Nadhani G8 ingekuwa bora. Nadhani kuirudisha Urusi lingekuwa jambo zuri. Tunatafuta amani duniani. Hatutafuti kucheza michezo."
Pendekezo la Trump la kuirejesha Urusi ndani ya kundi -- ambalo alilitolea mjini Washington muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda Canada -- lilikataliwa mara moja na wanachama wa G7 kutoka barani Ulaya, zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Ujerumani katika siku ya kwanza ya mkutano huo.
Urusi ilitimuliwa katika kundi lililokuwa wakati huo... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More