TTCL waahidi gawio kubwa zaidi kwa serikali mwaka 2019 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TTCL waahidi gawio kubwa zaidi kwa serikali mwaka 2019

SHIRIKA la Mawasiliano nchini (TTCL), limeahidi kutoa gawio kubwa zaidi kwa serikali mwakani, ili fedha hizo zikasaidie katika kazi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege vya serikali.Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba ambaye alitembelea banda la maonesho ya Kilimo la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, amesema wingi huo wa fedha utatokana na mashirika na taasisi za umma kuwaunga mkono kwa kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.“Mwaka huu tulitoa gawio la sh. Bil 5.1 kwa serikali, lakini ninaimani mwakani tutatoa zaidi endapo tutapata ushirikiano wa kutumiwa kwa huduma zetu kutoka kwenye taasisi nyingine za serikali, ambapo fedha hizo zinasambazwa na serikali kwenye kazi mbalimbali ukiwemo wa ujenzi wa viwanja vya ndege,” amesema Bw. Kindamba.Bw. Kindamba ameishukuru TAA kwa kuanza kutumia huduma ya mawasiliano ya simu kutoka kwenye shirika hilo, ambapo ita... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More