TUCTA YAKIRI KUSHIRIKISHWA MCHAKATO WA UTUNGWAJI WA KANUNI ZA MALIPO YA WASTAAFU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUCTA YAKIRI KUSHIRIKISHWA MCHAKATO WA UTUNGWAJI WA KANUNI ZA MALIPO YA WASTAAFU

Rais wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya amekiri shirikisho hilo kuwa na majadiliano mbalimbali katika ngazi ya Utatu na Upili yaani Serikali, Wafanyakazi na Waajiri kuhusu hoja ya kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi za jamii nchini. 
Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Morogoro leo sanjari na vikao vyao vya kikatiba takribani kwa siku mbili, Nyamhokya amesema wajumbe wamekuwa na fursa ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Ustawi wa Wafanyakazi nchini pamoja na kutoa tamko baada ya kuhudhuria kikao hicho rasmi cha utendaji wa maswala yanayotakiwa kufanyiwa utekelezaji.
Moja ya agenda zilizojadiliwa kwa undani ni swala la uunganiswaji wa wa mifuko ya hifadhi ya jamii na mkanganyiko uliojitokeza baada ya serikali kutangaza kuanza kutumika kwa vikokotoo vya mafao ya pensheni kwa wastaafu wa mifuko ya PSSSF na NSSF kuanzia Agosti 8 2018. Rais wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tuma... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More