TUCTA YAWATAKA WANASIASA KUTOWATUMIA KUJIPATIA UMAARUFU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUCTA YAWATAKA WANASIASA KUTOWATUMIA KUJIPATIA UMAARUFU

*Waziri Mkuu apokea maandamano ya wafanyakazi wakimpongeza Rais SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) limeyataka makundi ya wanasiasa kutowatumia wao kama njia ya kujitafutia umaarufu kwa kuzungumzia masuala yao na badala yake wawaachie viongozi wa vyama hivyo kwa sababu wanajitosheleza.
 Pia shirikisho hilo limesema litaendelea kuiunga mkono na kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano pamoja na rais wake Dkt. John Magufuli na kwamba watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya ajira zao.
Hayo yamesemwa leo (Jumatatu, Januari 7, 2019) na Katibu Mkuu wa TUCTA, Yahya Msigwa katika hotuba yake aliyoitoa kwa wafanyakazi baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kupokea maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi.
Watumishi wa taasisi mbalimbali leo wameandamana jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Squarekwa lengo la kumpongeza Rais Dkt. Magufuli kwa uamuzi wake kufuta kikotoo kipya cha mafao ya wafanyakazi kilichopendekezwa katika kanuni za sheria ya Mifuko ya j... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More