TUHUMA ZA RUSHWA KATIKA KUICHAGUA QATAR KUWA MWENYEJI KOMBE LA DUNIA 2022 KWAMWEKA HATIANI PLATIN - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUHUMA ZA RUSHWA KATIKA KUICHAGUA QATAR KUWA MWENYEJI KOMBE LA DUNIA 2022 KWAMWEKA HATIANI PLATIN

Na Leandra Gabriel, Blogu ya JamiiALIYEKUWA  Rais wa shirikisho la mpira barani Ulaya (UEFA) kwa mwaka 2007-2015, mchezaji wa zamani wa Ufaransa na mshindi mara tatu wa tuzo ya Ballon I'or Michel Platini anahojiwa na mamlaka za uchunguzi wa masuala ya ufisadi na rushwa kwa kile kilichoelezwa ni kuipa nafasi Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la duniani mwaka 2022 vyombo vya habari nchini Ufaransa vimeripoti.
Michel (63) ambaye aliwahi kuwa Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya na baadaye kufungiwa kujihusisha na soka mwaka 2015 kwa kile kilichoelezwa ni ukiukwaji wa kanuni maadili.
Wakati wa kutafuta mwenyeji wa mashindano hayo ya kidunia mwaka 2010 Qatar iliibwaga Marekani, Australia, Japan na Korea Kusini. Michel amekana mashtaka hayo aliyohojiwa huko Nanterre magharibi wa mji mkuu wa nchi hiyo Paris.
Imeelezwa kuwa shutuma dhidi yake zilianza kuchunguzwa miaka miwili iliyopita na katika sakata hilo Sepp Blatter aliyewahi kuwa Rais wa shirikisho la mpira duniani (FIFA) ambaye pia alipigwa m... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More