TULIYOKUBALIANA SADC YAKITEKELEZWA YATALETA MANUFAA MAKUBWA KWA NCHI WANACHAMA-DK MAGUFULI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TULIYOKUBALIANA SADC YAKITEKELEZWA YATALETA MANUFAA MAKUBWA KWA NCHI WANACHAMA-DK MAGUFULI

Na Leandra Gabriel,Michuzi TV
MWENYEKITI wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli amesema kuwa agenda na maazimio yaliyopatikana kupitia mkutano huo yakitekelezwa kwa vitendo yataleta manufaa makubwa kwa nchi wanachama.
Akizungumza katika ufungaji wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Rais Magufuli amesema kuwa mkutano huo umekuwa wa mafanikio makubwa na wamefikia makubaliano katika masuala mbalimbali ikiwemo kuwekeza katika viwanda ili kufikia azma iliyowekwa 2015)2063 na hiyo ni pamoja na kuboresha mazingira, kutoweka vikwazo katika mipaka, kupambana na ukiritimba katika maamuzi pamoja na kupambana na rushwa huku akieleza mambo hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi ndani ya jumuiya hiyo.
Aidha katika mkutano huo wakuu wa nchi wamedhamiria kushirikiana katika kudumisha amani katika nchi ya Jamhuri ya Kongo pamoja na kuunda chombo ma... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More