TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YAKABIDHI RIPOTI YA MAPENDEKEZO SHERIA YA UFILISI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YAKABIDHI RIPOTI YA MAPENDEKEZO SHERIA YA UFILISI

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Balozi Augustine Mahiga amepokea ripoti ya mapendekezo ya sheria yaliyowasilishwa na Tume ya Kurekebisha Sheria hii leo Jijini Dodoma.
Akipokea taarifa hiyo Dkt Balozi Mahiga amefurahishwa kwa kazi nzuri iliyofanywa na Tume hiyo pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha kukamilika kwa mapendekezo ya sheria ya Ufilisi na nyingine zilizowasilishwa katika tume hiyo  ambazo ni sheria ya Ushahidi na ile ya Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro.
‘’Nimeridhishwa kwa kazi nzuri iliyofanyika kwani tunakwenda kupata sheria madhubuti itakayoendana na hali ya sasa na kusimamia kikamilifu misingi ya utawala bora’’. Alisema Balozi Mahiga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Mhe, Januari  Msofe amesema kuwa tume yake imefanya mapitio na utafiti wa kina kuhusu mifumo ya  Sheria zinazosimamia Ufilisi na kubaini mapungufu ya kisheria na kiutendaji ambao umeathili utekelezaji wa masuala ya hayo hapa Nchini.
Ameendelea kubainisha mapungufu hayo ni pa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More