TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA YAWASHAURI WAFANYABIASHARA KUPIMA BIDHAA ZAO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA YAWASHAURI WAFANYABIASHARA KUPIMA BIDHAA ZAO

TUME  ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) imewashauri wafanyabiashara nchini kuendelea kupima bidhaa zao ili kuhakikisha mionzi yake ni salama na ambayo haitaleta madhara.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Busagala alipowasilisha mada katika mkutano wake na baadhi ya wafanyabiashara wa jijini Mwanza ambapo amesema kwa kupima bidhaa zao ni jambo la kufuata sheria.
  Pia amezungumza nao kuhusu majukumu ya tume kisheria ili kuongeza uelewa na kujadiliana hatua mbalimbali ambazo zitaisaidia kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Mwanza na wafanyabiashara wote wanaolizunguka ziwa Victoria.
 
Katika mkutano huo ,wamejadili masuala mbali mbali ya Tume ya Atomiki Tanzania ikiwa ni pamoja na kuangalia mapungufu mbalimbali na hatimaye kuchukua hatua stahiki ili kuweka ustawi mzuri kati ya wafanyabiashara wa Mwanza na maeneo menginine nchini na kuyafanyia kazi kwa lengo la uboreshaji.

Tume ya Nguvu za Atomiki Ta... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More