TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI YATAKIWA KUHAKIKI ENEO LINALOFAA KWA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI YATAKIWA KUHAKIKI ENEO LINALOFAA KWA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI.

Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ishirikiane na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali na wataalam kutoka chuo kikuu cha ardhi kuhakiki eneo lenye ukubwa wa hekta 475,052 liloripotiwa na Tume hiyo kuwa linafaa kwa kilimo cha Umwagiaji nchini. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Mgumba ameyasema hayo alipofanya ziara katika ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam ili kuongea na watumishi, ambapo aliwataka wao kama Tume washiriki kwanza kuhakiki eneo hilo na kuweza kutoa taarifa za uhakika. 
“Mnaweza kushirikiana na ofisi za kanda na halmashauri ili kuweza kurahisisha kufanyika kwa kazi hii , kwenye kilimo ni vyema tukaenda na mambo yote matatu, kilimo cha kutegemea maji ya mvua, kiimo cha kutegemea maji ya ardhini na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji cha kutumia miundombinu, kilimo ambacho kitatuhakikishia uhakika wa chakula kwani ni kilimo ambacho mkulima analima zaidi ya mara moja kwa mwaka.” Alisema Naibu Waziri. 
Sambamba na hilo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More