TUMEJIDHATITI KUPUNGUZA FOLENI ENEO LA TAZARA- MHANDISI MFUGALE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUMEJIDHATITI KUPUNGUZA FOLENI ENEO LA TAZARA- MHANDISI MFUGALE

Na Paschal Dotto-MAELEZOSerikali Kupitia Wakala wa Barabara TANROADS  leo imesimamia zoezi la kuanza majaribio ya kutumia  Barabara za juu flyover zilizoko katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere,  ambazo ujenzi wake umemalizika hivi karibuni.
Zoezi  hilo ambalo lilianza saa 3:00 asubuhi limepokelewa vyema na waendesha magari na wananchi kwa ujumla na majira ya saa sita mchana eneo la TAZARA limeonekana tupu huku watazamaji wakishangaa na nyuso zao kuonekana za furaha kwa kazi nzuri ya Serikali yao.
Kuanza kutumika kwa barabara za juu eneo hilo la TAZARA kunafuta mlundikano wa magari ya mizigo toka bandarini kwenda mikoani na abiria wa ndege waingiao na kutoka Uwanja wa kimataifa Dar es Salaam  kutumia muda mwingi kwenye barabara za Nyerere na Mandela hadi saa moja au zaidi badala ya dakika 20 za sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa TANROAD Mhandisi Patrick Mfugale, ameeleza kuwa barabara hizo ziko tayari kwa matumizi kwa waendeshaji wa magari jijini... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More