TUMEJIDHATITI KUPUNGUZA FOLENI ENEO LA TAZARA- MHANDISI MFUGALE - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUMEJIDHATITI KUPUNGUZA FOLENI ENEO LA TAZARA- MHANDISI MFUGALE


Magari yakipita kwa ajili ya majaribio leo (Jumamosi septemba 15, 2018 barabra za juu flyover ya Mhandisi Patrick Mfugale lililopo eneo la TAZARA Jijini Dar es Salaam ambalo hivi karibuni linatarajiwa kufunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli. Picha na Paschal Dotto –MAELEZO


Na Paschal Dotto-MAELEZOSerikali Kupitia Wakala wa Barabara TANROADS  leo imesimamia zoezi la kuanza majaribio ya kutumia  Barabara za juu flyover zilizoko katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere,  ambazo ujenzi wake umemalizika hivi karibuni.
Zoezi  hilo ambalo lilianza saa 3:00 asubuhi limepokelewa vyema na waendesha magari na wananchi kwa ujumla na majira ya saa sita mchana eneo la TAZARA limeonekana tupu huku watazamaji wakishangaa na nyuso zao kuonekana za furaha kwa kazi nzuri ya Serikali yao.
Kuanza kutumika kwa barabara za juu eneo hilo la TAZARA kunafuta mlundikano wa magari ya mizigo toka bandarini kwenda mikoani na abiria wa ndege ... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More