TUMETOA ELIMU YA KUTOSHA KWA WANANCHI JUU YA UPOKEAJI WA FEDHA ZA KOROSHO-Mkurugenzi Newala. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUMETOA ELIMU YA KUTOSHA KWA WANANCHI JUU YA UPOKEAJI WA FEDHA ZA KOROSHO-Mkurugenzi Newala.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii,Newala ,Mtwara.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae amesema tangu kutangazwa kwa operesheni korosho ofisi yake kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Newala wamezunguka  Wilaya nzima kutoa elimu kuhusu nini kifanyike kupitia agizo la Rais Magufuli kuwa Serikali itanunua Korosho yote nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake Wilayani Newala Chimae amesema kuwa  wamezunguka kwa wananchi kutoa elimu juu ya namna zoezi hilo litakavyoendesha ikiwa ni pamoja na kuwataka watendaji wa vijiji na kata kusimamia zoezi hilo kwa makini hili kusitokee malalamiko yoyote."Sambamba na zoezi la uhakiki wa taarifa za wakulima pia tumetoa maagizo kwa watendaji wa mitaa na kata kusimamia zoezi la uingizaji wa korosho kwenye maghala na kuhakikisha kuwa hakuna korosho inayoingia kutoka nje ya mitaa au kata zao ili kudhibiti korosho za magendo zinazoingizwa kutoka nchi jirani," alisema Chimae.
amesema kuwa Halmashauri... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More