TUMEVUNA TULICHOPANDA, TUELEKEZE NGUVU KWENYE MCHEZO WA MARUDIANO TULIPE KISASI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUMEVUNA TULICHOPANDA, TUELEKEZE NGUVU KWENYE MCHEZO WA MARUDIANO TULIPE KISASI

TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars juzi imepata kipigo cha kushitua cha mabao 3-0 kutoka kwa wenyeji, Cape Verde katika mchezo wa Kundi L  kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Praia.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa wa Mali, Boubou Traore, Drissa Kamory Niare na Baba Yomboliba, mabao yaliyoizamisha Taifa Stars leo yalifungwa na mshambuliaji wa klabu ya Partizan ya Ligi Kuu ya Serbia, Ricardo Jorge Pires Gomes na beki wa MOL Vidi FC ya Hungary Ianique dos Santos Tavares maarufu kama Stopira.
Kwa matokeo hayo, Cape Verde imefikisha pointi nne, sasa ikishika nafasi ya pili kwenye Kundi L, nyuma ya Uganda  yenye pointi saba, wakati Leshoto na Tanzania zinafuatia. 
Huo utakuwa mchezo wa tatu wa Taifa Stars katika kundi bila ushindi, baada ya awali kutoa sare za 1-1 na Lesotho Dar es Salaam na 0-0 na Uganda mjini Kampala.
Kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike akiiongoza Taifa Stars kwa mara ya pili leo tangu aanze kazi Agosti alifanya ... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More