TUMIENI MASHABIKI KUJIJENGA KIUCHUMI-MAJALIWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUMIENI MASHABIKI KUJIJENGA KIUCHUMI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amevitaka vilabu vya soka nchini kutumia vema fursa ya kuwa na mashabiki wengi katika kuvifanya viweze kujitegemea kiuchumi.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 15, 2019) katika hafla ya kuchangia klabu ya Yanga, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.Ameichangia klabu hiyo sh. milioni 10.
“Natambua kwamba Yanga ni klabu kubwa na kongwe nchini ikiwemo Simba Sport Club ambazo ndizo zina wanachama na mashabiki wasiopungua milioni 20 au zaidi.” 
Hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuvitaka vilabu vya soka nchini kutafuta njia nzuri na endelevu ya kupata mapato ili kuendesha timu zao na kujiimarisha kiuchumi. 
Amesema kwamba, kuimarika kwa vilabu hivyo vyenye ushawishi mkubwa katika soka nchini ni muhimu kwa mustakabali wa soka la Taifa letu. Waziri Mkuu amesema kufanya vizuri kwa vilabu hivyo kuna uhusiano wa mkubwa na wa moja kwa moja na mafanikio ya timu ya soka ya Taifa.
“Nampongeza kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kwa k... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More