TUNAONA KAMA TAIFA STARS IMEKWISHAFUZU FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA MWAKANI NCHINI CAMEROON, WAKATI... - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUNAONA KAMA TAIFA STARS IMEKWISHAFUZU FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA MWAKANI NCHINI CAMEROON, WAKATI...

TANZANIA imefufua matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Cameroon kufuata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde kwenye mchezo wa Kundi L Jumanne Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Ushindi huo ulikuja siku tatu baada ya Taifa Stars kufungwa mabao 3-0 na Papa wa Bluu katika mchezo wa kwanza mjini Praia Oktoba 12 na kuwatia simanzi kubwa Watanzania.
Ushindi huo wa kwanza kwenye mashindano haya, unaifanya Taifa Stars ijisogeze hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo, ikifikisha pointi tano baada ya kucheza mechi nne, ikifungwa moja na sare mbili. 
Uganda ambayo siku hiyo iliifunga tena Lesotho 2-0 mjini Maseru, ndiyo inaongoza kundi hilo kwa pointi zake 10 za mechi nne, wakati Cape Verde inabaki na pointi zake nne katika nafasi ya tatu. Lesotho ndiyo inashika mkia kwa pointi zake mbili. 


Shujaa wa Tanzania Jumanne alikuwa Nahodha Mbwana Ally Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji aliyefunga bao moja na kuseti moja katika ushindi huo,... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More