TUNATEKELEZA KAULI YA RAIS DKT MAGUFULI YA TANZANIA YA VIWANDA-TROPICAL INDUSTRIES - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUNATEKELEZA KAULI YA RAIS DKT MAGUFULI YA TANZANIA YA VIWANDA-TROPICAL INDUSTRIES

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
KIWANDA Cha Wazalendo cha Tropical Industies wamemshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapa fursa wamiliki wa viwanda ambao ni wazalendo kuuza bidhaa zao kwa urahisi mkubwa.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Charles Mlawa katika maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Michuzi TV, Mlawa amesema kiwanda chao kinajishugulisha na utengenezaji wa transfoma, nyaya za umeme za usambazaji na nyaya za usafirishaji zikizalishwa hapa nchini.
Mlawa amesema, amemshukuru Rais kwa fursa aliyoitoa kwa wazalendo kuweza kufanya biashara kwani kipindi cha nyuma walijaribu kufanya jitihada za kuuza kwa wateja wa ndani ilishindikana.
“Kauli ya Rais ya Tanzania ya Viwanda kuelekea uchumi wa kati imesaidia sana,wao kama kiwanda wamenufaika kwa kupata wateja wa ndani na nje ya nchi,”amesema Mlawa.
Aidha, amesema ndani ya miaka mine ya Dkt John Pombe Magufuli kwa vitendo na kwa kuzalis... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More