Tunda Afunguka Kuhusu Tetesi Za Kuwa na Mpenzi Mpya - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tunda Afunguka Kuhusu Tetesi Za Kuwa na Mpenzi Mpya

Video vixen maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Tunda Sebastian amefungukia tetesi za kuwa na njemba mpya na kuweka wazi kuwa yule ni rafiki tu hana Mahusiano naye.


Wiki iliyopita taarifa zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Tunda na mpenzi wake wa Miezi kadhaa Mtanagzaji Casto Dickson wameachana na mara moja kuna taarifa zilidai kuna mpenzi mpya.


Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Tunda alisambaza screenshot ya FaceTime na mwanaume mwingine picha iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha kusambaa kwa Taarifa kuwa Tunda ana mpenzi mpya.


Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Vibes, Tunda amesema mwanaume huyo aliyekuwa anachati naye ni rafiki yake wa kawaida tu na siyo mpenzi wake kama watu wanavyodai.Jamani nawashangaa sana watu maana siyo kila ninayeongea naye ni mpenzi wangu, huyu ni rafiki yangu tu wa kawaida hivyo nawasihi watu wasiwe na tafsiri za mapenzi tu kila wakati“. 


The post Tunda Afunguka Kuhusu Tetesi Za Kuwa na Mpenzi Mpya appeared first ... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More